Yanga yanasa kiungo mkabaji kutoka Zambia


Timu ya Yanga chini ya kocha George Lwandamina huenda ikamaliza tatizo la kiungo mkabaji kwenye timu hiyo baada ya Justice Zulu kutua nchini.

Zulu ambaye n raia wa Zambia huenda akasini rasmi Yanga kati ya leo au kesho na kuungana na chama hilo la jangwani.

Tayari timu ya Yanga imeanza mazoezi chini ya Lwandamina ambaye tayari amefanikisha mpango wa kumleta kiungo huyo ili kuongeza nguvu kwenye ligi na mechi za kimataifa.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zimethibitisha kuwa nyota atasaini muda wowote kuanzia sasa kwa kuwa kila kitu kipo tayari.

Comments