Timu ya Mbeya leo katika uwanja wa Sokoine imewaacha mdomo wazi mashabiki wa Yanga baada ya kuifunga timu hiyo bao 2-1.
Yanga yenye pointi 27, imepoteza mchezo wa pili baada ya kufungwa na Stand united hapo awali katika uwanja wa Kambarage.
Matokeo hayo huenda yakawa shangwe kwa upande wa wapinzani wao Simba ambao wameshinda mechi yao dhidi ya Stand united na kuiacha Yanga pointi 8.
Yanga ambayo ilipata mfululizo wa matokeo kwenye mechi nne zilizopita ina kibarua kizito cha kukabiliana Prisons katika mechi ijayo.

Comments
Post a Comment