Timu ya Simba imeamua kuachana wachezaji wake wawili akiwemo golikipa Vicent Angban pamoja na mshambuliaji Fredrick Blagnon.
Kamati ya usajili ya Simba kwa pamoja iliridhia maamuzi hayo ya kuachana wachezaji wageni hao ili kupisha usajili wachezaji Agyei pamoja James Kotei.
Kwa upande mwingine Simba imeamua kumtoa kiungo wao Ndusha kwa mkopo katika moja ya timu ya Oman.
Simba imeamua kufanya marekebisho kwenye kikosi chao ili kulinda nafasi ya kupigania ubingwa msimu huu.

Comments
Post a Comment