Azam, Simba kutimua vumbi viwanjani Leo


Timu ya Simba na Azam kwa pamoja zitashuka viwanja tofauti kuanza raundi ya pili ya ligi kuu leo.

Azam itakuwa mgeni wa African Lyon katika uwanja wa Uhuru wakati Simba itakuwa mgeni wa Ndanda katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Tayari ligi ilishaanza jana ambapo Yanga iliweza kuikaribisha JKT Ruvu na kipigo baada ya kuifunga bao 3-0 katika uwanja wa Uhuru.

Kwa upande mwingine timu ya Mwadui FC katika uwanja wa Mwadui Complex iliweza kuilaza Toto Africans bao 1-0.

Comments