Timu ya Barcelona ipo kwenye mipango ya kumpatia mkataba mpya Luis Suarez hadi mwaka 2022.
Suarez mwenye miaka 29 alichukua kiatu cha dhahabu msimu uliopita baada kutumbukiza mabao 40 katika ligi ya Spain (La liga).
Uwezo mkubwa uliooneshwa na mfumania nyavu huyo wa Uruguay umeingoza Barcelona kutetea ubingwa wao msimu uliopita.
Muungano wa Messi, Suarez na Neymar (MSN) uliweza kuzaa jumla ya mabao 131 katika mashindano yote ambayo Barcelona ilishiriki mwaka 2015/16.
Barcelona kupitia Rais wake Bortameu imeweka wazi nia yao ya kumuongeza mkataba mpya Suarez ambaye anatisha katika tasnia ya soka duniani.

Comments
Post a Comment