Beki wa kulia wa klabu ya Arsenal Hector Bellerin atarejea kwenye kikosi cha timu hiyo dhidi ya Stoke city wikiendi hii.
Bellerin alikosa mechi 6 ambazo Arsenal ilicheza tangu alipoingia kwenye jereha la goti Novemba 17 mwaka huu.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema kuwa Bellerin anaendelea vizuri na hivyo atarejea katika mechi dhidi ya Stoke city wikiendi hii.
"Anaendelea vizuri na sasa yupo kamili tunategemea kuwa kuwa naye katika mechi na Stoke city." Alisema Wenger
Mbali na Bellerin pia mshambuliaji Danny Welbeck pamoja na kiungo Santi Carzola wanaendelea vizuri na tayari wameshaanza mazoezi mepesi.

Comments
Post a Comment