Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema ameingia kwenye orodha ya wafungaji 6 bora katika ligi ya mabingwa barani Ulaya (UCL).
Benzema aliifungia timu yake mabao 2 katika mechi ya jana dhidi ya Dortmund na kufikisha jumla ya goli 50 alizofunga kwenye ligi hiyo.
Mshambuliaji huyo anaungana na mfaransa mwenzie Thiery Henry ambaye pia amefunga idadi hiyo ya mabao kwenye michuano hiyo.
Hadi sasa Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Raul Gonzalez na Rud van Nestelrooy ndiyo pekee waliofunga mabao mengi kwenye michuano hii.

Comments
Post a Comment