Timu ya Chelsea imeonesha kuwa haishikiki msimu baada ya kuifunga Manchester city bao 3-1 katika uwanja wa Etihad.
City ilianza kupata goli kupitia Gary Cahil ambaye alijifunga hata hivyo Vijana hao wa Antonio Conte waliweza kuchomoa bao hilo kupitia Diego Costa, na kufunga mengine wawili kupitia Willian na Eden Hazard.
Chelsea ambao walicheza kwa nidhamu ya hali ya juu wameendelea kujihakikishia kuongoza kwenye msimamo wa ligi ya England ikiwa imekusanya pointi 34 kwenye mechi 14.
Conte ameendelea kutamba katika ligi ya England tangu alipoanza kutumia mfumo wa 3-4-3.

Comments
Post a Comment