Dortmund yaigomea Madrid kwa Aubemiyang


Bosi wa Borrusia Dortmund Thomas Tuchel amesema mshambuliaji wa timu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang hauzwi kwenda popote.

Tuchel alisema kuwa ni ngumu kumuuza mshambuliaji anayefanya vizuri kwenye timu, tangu aliposajiliwa.

"Ni ngumu sana kumuuza mchezaji anayefanya vizuri kwenye timu, hii salamu kwa Real Madrid kwamba hatutawauzia Aubameyang." Alisema bosi huyo

Mshambuliaji huyo ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika mwaka Jana ameifungia timu hiyo magoli magoli 69 katika mechi 108 alizoichezea Dortmund.

Comments