Timu ya Everton jana imefanikiwa kuituliza Arsenal baada ya kuwachapa bao 2-1 katika uwanja wa Goodson Park.
Arsenal ilianza kupata bao kupitia Alexis Sanchez aliyefunga dakika ya 12, hata hivyo Seamus Coleman alichomoa bao hilo dakika ya 43, na kipindi cha pili Ashely williams alifunga bao la ushindi.
Michezo mingine itaendelea siku ya leo ambapo Middlesbrough wataikaribisha liverpool nyumbani, Chelsea watakaribishwa na Sunderland na Man utd dhidi ya West Brom.

Comments
Post a Comment