Fabrigas: Nimeanza kumsoma Conte


Licha ya mwanzo mgumu katika kikosi cha Chelsea Cesc Fabrigas amesema kuwa kwa sasa ameanza kuusoma mtindo wa Antonio Conte.

Fabrigas ambaye alianza vibaya katika timu ya Conte alisema kuwa kwa sasa hakuna kinachoshindikana kwenye mfumo huo.

"Nimeanza kupata mfumo huu vilivyo, mwanzo ilikuwa ngumu kwangu lakini kwa sasa kila kitu kimekuwa sawa, hakuna gumu tena kwenye mfumo wa Conte.

"Nadhani nina wakati mzuri kwa sasa, nina pata raha  kucheza juu ya N'golo Kante na Nemanja Matic hii hunifanya nitafute nafasi kwa ajili ya kupiga pasi uwanjani." Alisema Fabrigas

Fabrigas alifunga bao la pekee la ushindi katika mechi dhidi ya Sunderland iliyochezwa juzi katika uwanja wa Light.

Comments