Hanspope: Simba haitambeleza mchezaji


Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Zacharia Hanspoppe amesema kuwa timu hiyo haitishiwi nyau na mchezaji mmoja.

Simba inajiandaa kumalizana na James Kotei ambaye ametokea nchini Ghana ili kuchukua nafasi ya Jonas Mkude.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa ingawa timu hiyo imeyumba kiuchumi lakini haishindwi kusajili mchezaji inayomtaka.

"Hatuna muda wa kubembeleza mchezaji, tumeshusha kiungo kutokana Ghana iwapo kocha ataridhia kiwango chake tutampa mkataba wa miaka 2." Alisema Hans

Mkude aligomea mkataba mpya Simba kutokana na madai ya kuwepo kwa mkabata wa ambao unapunguza maslahi yake.

Comments