Baada ya kuchezwa kwa mechi za robo fainali ya kombe la ligi (EFL) nchini England hatimaye Man utd, Liverpool, Hull city na Southampton zatinga nusu fainali.
Liverpool itachuana na Saints ambao wamewaondoa Arsenal jana katika uwanja wa Emirates, na Man utd itakutana Hull city baada ya kuiburuza West Ham bao 4-1.
Mechi zote zitachezwa nyumbani na ugenini kama ilivyo taratibu na kanuni za kombe hilo ambalo huandaliwa kila mwaka.

Comments
Post a Comment