Wladimir Klitschko anaamini kipigo alichopokea kutoka kwa Tyson Fury katika mpambano wake wa mwisho utamfanya kuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Anthony Joshua.
Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu, atakuwa kipimo kizuri kwa bingwa wa IBF ambaye amepigana mapambano 18 katka pambano la April 29 litakalofanyika katika uwanja wa wembley
Klitschko, amesisitiza kuwa kupoteza ubingwa
wake kwa Fury umemtia hamasa kitu ambacho kinamaanisha ni shida kwa Joshua.
Klitschko (64-4) ni bingwa wa zamani wa
mikanda ya IBF anaoushikilia sasa Joshua, pamoja na WBA na WBO, hajapanda
ulingoni tangu apoteze mikanda hiyo kwa Tyson Fury.

Comments
Post a Comment