Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameachana na mpango wa kumuuza Daniel Sturridge hadi kipindi cha majira ya joto hapo mwakani.
Sturridge mwenye miaka 27 aliweka wazi nia yake ya kuachana na Liverpool kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Mjermani huyo.
West Ham ndiyo waliokuwa wanaongoza kwenye mbio za kumwania mchezaji huyo ambaye alionesha nia ya kutimka Anfield katika dirisha dogo la usajili mwezi January.
Kuumia kwa Phelipe Coutinho huenda kumemfanya Klopp kutengua maamuzi yake kwa ajili ya kujipanga na ushindani wa kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea ameshindwa kuungana na wenzake mazoezini kutokana na jeraha la goti linalomkabili mara kwa mara.

Comments
Post a Comment