![]() |
| TP Mazembe ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo. |
Serikali
ililitaka shirikisho la soka nchini humo kusitisha mechi za ligi kuanzia
Alhamisi.
Hatua
hiyo imetokea huku wasiwasi ukiendelea kwamba huenda kukatokea vurugu muhula wa
Rais Joseph Kabila utakapofikia kikomo wiki ijayo.
"Hali
iliyopo nchini huenda ikafika viwanjani," Barthelemy Okito, katibu mkuu wa
wizara ya michezo alisema.
Majuzi wakati wa
mechi, mashabiki walisikika wakiimba kwamba muhula wa Kabila unamalizika.
Kabila
alitakiwa kung'atuka 19 Desemba lakini amesema anapanga kusalia madarakani hadi
Aprili 2018, wakati ambao serikali inasema itaweza kufanya uchaguzi ambao
ulikuwa umepangiwa kufanyika mwezi jana.

Comments
Post a Comment