Liverpool yafanya balaa EPL, yaikalisha Stoke city 4-1.


Licha ya kumkosa nyota wao Phelipe Coutinho Liverpool imeibuka na ushindi wa bao 4-1 hapo jana.

Stoke city ambayo ilianza vizuri dakika za awali ilipata bao la kuongoza kupitia Walters, hata hivyo Liverpool ilichomoa bao hilo kupitia Adam Lallana na kuongeza bao la pili kabla ya kwenda Half time.

Kipindi cha pili Liverpool iliweza kukamilisha idadi ya pointi 3 baada ya kuongeza bao mbili zingine ambazo zilifungwa na Daniel Sturridge na bao lingine alijifunga kiungo wa Stoke city Imbula.

Matokeo hayo yanaingoza Liverpool kusimama nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu England ikiwa na jumla  ya pointi 40.

Comments