Timu ya Liverpool jana imebuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodson Park.
Liverpool ilipata bao la ushindi kupitia mshambuliaji wake Sadio Mane aliyefunga dakika 90 zikiwa zimesalia dakika chache mpira umalizike.
Mechi hiyo ya watani wa jadi ilitawaliwa na upinzani mkali katika vipindi vyote viwili licha ya Liverpool kutawala zaidi mpira kipindi cha pili.
Daniel Sturridge aliyetokea benchi alichangia kupatikana kwa bao hilo baada ya kupiga mpira uliogonga mwamba na kumwezesha Sadio Mane kupasia nyavu.

Comments
Post a Comment