Mbuyu Twitte afungashiwa virago vyake, Mkude anukia Jangwani



Klabu ya Yanga imeamua kuachana rasmi na Mbuyu Twitte baada ya usajili wa Justice Zulu.

Hivi karibuni Yanga ilimsajili kiungo kutoka Zesco ya Zambia Justice Zulu na hivyo hakuna nafasi kwa beki huyo ambaye pia hucheza nafasi ya kiungo.

Zipo tetesi kuwa Yanga inaweza kumsajili kiungo wa Simba Jonas Mkude ambaye hana maelewano mazuri na viongozi wa timu yake.

Zipo dalili kuwa huenda Mkude akatua Yanga baada ya Simba kuweka wazi nia yake ya kusajili kiungo mkabaji mwingine kutokana na malingo ya Mchezaji huyo.

Simba na Yanga zimeendelea kujipanga kwa namna tofauti ili kuongeza nguvu na ushindani katika ligi ya Vodacom.

Comments