Mshahara wamrudisha mkude mazoezini


Kiungo wa Simba Jonas Mkude hatimaye arejea mazoezini baada ya kushindwa kuungana na wenzie kwa siku nne.

Mkude aligoma kufanya mazungumzo ya kujadili mkataba mpya na Simba tangu alipohitajika kukutana na viongozi wa timu hiyo kama ilivyokuwa kwa Mohammed Hussein.

Simba ilitishia kumkata mshahara nyota huyo ambaye ameonekana mazoezini punde baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka kwa viongozi wake.

Hadi sasa haijulikani kwanini kiungo huyo mkabaji ambaye amekuwa muhimili wa simba kwa miaka 2 sasa kugomea kusaini mkataba mpya.

Comments