Mchezaji Hamis Riphat kutoka Ndanda FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom kwa mwezi Novemba.
Nyota huyo aliwashinda Shaban Idd pamoja Mbaraka Abeid wa Kagera Sugar ambao walikuwepo kwenye kinyanganyiro hicho.
Riphat aliifungia ndanda magoli mawili katika mechi alizoichezea Ndanda mwezi Novemba na kuingoza kukusanya pointi 6 ambazo zimeiwezesha Ndanda kumaliza nafasi ya 10 kwenye Raundi ya kwanza.
Mchezaji huyo atakabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja na Kampuni ya Vodacom ambayo inadhamini ligi kuu baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Comments
Post a Comment