Timu ya Manchester city imetoka na pointi 3 mbele ya Arsenal baada ya kuichapa 2-1 katika uwanja wa Etihad.
Katika pambano hilo city iliwakosa wachezaji wake mahili akiwemo Kun Aguero pamoja na Fernandinho ambao wanatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Licha ya kuwakosa nyota hao lakini mshambuliaji Leroy Sane na Reheem walitosha kumlaza Wenger vibaya baada ya kulifuta bao la Theo Walcott aliyeitanguliza Arsenal kipindi cha kwanza.
City ikiwa imewakosa Aguero na Fernandinho imeweza kubeba pointi 6 baada ya kuwafunga Watford na Arsenal.

Comments
Post a Comment