Ranieri: Siogopi kutimuliwa Leicester city


Kocha wa Leicester city Claudio Ranieri amesema kuwa hana hofu ya kutimuliwa na mmiliki wa hiyo.

Kauli hiyo aliitoa Ranieri kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata.

Kocha huyo aliweka wazi kuwa bosi wa timu hiyo Vichai Srivadhannaprabha harizishwi na mwenendo wa timu hiyo jinsi ulivyo hadi sasa.

Leicester city maarufu kama "Foxes" waliushangaza ulimwengu baada ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu England ikiwa ni msimu mmoja mbele baada ya kupanda daraja.

Comments