Baada ya Tevez kuvuta mpunga kwenye ligi ya China na duniani kwa sasa hatimaye wachina wahamia kwa Christiano Ronaldo.
Moja ya timu zinazoshiriki ligi ya China ambayo jina lake halijawekwa wazi imepanga kumlipa Ronaldo mshahara usiopungua £85 milioni kwa mwaka.
Hayo yamesemwa na wakala wa mchezaji huyo George Mendez ambaye amepokea ofa hiyo hivi karibuni.
Timu hiyo imetoa ofa ya £256 milioni kwa Real Madrid kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo bora duniani kwa mwaka 2016.

Comments
Post a Comment