Sanchez apiga hat trick, Arsenal ikiua 5-1


Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez amefunga hat trick katika ushindi wa bao 5-1 dhidi ya West Ham.

Sanchez alifunga bao hizo katika dakika ya 72, 80 na 86 na mabao mengine yakifungwa na Mesut Ozil dakika ya 24 pamoja na Oxlade Chamberlain.

Mabao hayo yamemsogeza Sanchez kwa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ambaye ametikisa nyavu mara 11 hadi sasa.

Comments