Simba: Twitte hayupo kwenye mipango yetu


Klabu ya Simba imesema kuwa haina mpango wa kumsajili Mbuyu Twitte kama inavyodhaniwa.

Hayo yamesemwa na makamu mwenyekiti wa timu hiyo Geofrey Nyange 'Kaburu' ambaye amekanusha taarifa hizo.

Kiongozi huyo alisema kuwa mipango ya Simba ni kusajili wachezaji wazawa ambao muda wowote kuanzia watasaini na kutangazwa timu hiyo.

"Hatuna mipango na Mbuyu Twitte, tupo njiani kusajili wachezaji wa wazawa ambao tutawatangaza.

"James kotei anaendelea vizuri hivyo tunaangalia taratibu za kumalizana nae, endapo mwalimu ataridhia." Alisema kaburu

Comments