Kocha wa Yanga George Lwandamina amevutiwa vilivyo na kiwango cha Amis Tambwe na hivyo amempa mkataba mpya hadi 2019.
Uwezo mkubwa wa kufumania nyavu ambao umeoneshwa na mrundi huyo umemshawishi Lwandamina kuomuongeza Tambwe miaka 2 kwenye mkataba wake.
Tambwe ambaye amefunga magoli 8 hadi sasa rasmi amekuwa mali ya Yanga baada ya kumwaga wino miaka 2.
"Najisikia furaha kwa kuwa Yanga n mahali sahihi kwangu, naahid kuendelea kuwapa raha mashabiki ambao wakati wamekuwa nami." Alisema Tambwe baada ya kusaini mkataba

Comments
Post a Comment