Tetesi: Fonte anukia Man utd


Beki kisiki wa Ureno Jose Fonte huenda akatua Manchester united kwenye dirisha dogo la usajili mwezi January.

Fonte mwenye miaka 32 ameshindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na Southampton hivyo huenda njia ikawa nyeupe kwa Jose Mourinho ambaye amwekuwa akimfukuzia Mreno huyo.

Kocha wa Man utd Jose Mourinho anavutiwa na mpango wa kumsajili beki huyo ambaye aling'aa kwenye michuano ya UEFA Euro na kuingoza Ureno kutwaa taji hilo.

Kuumia kwa Eric Baily inaweza kuwa chachu ya kumfanya kocha Jose Mourinho kumalizana na Fonte haraka iwezekanavyo ili kukabiliana na ushindani mkali wa EPL.

Comments