Beki aliyetemwa Yanga Mbuyu Twitte huenda akajiunga na Simba kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Twitte aliachia nafasi Yanga ili kupisha usajili wa Kiungo Justice Zulu aliyetoka Zesco ya Zambia.
Beki huyo amefanya mazungumzo na Rais wa Simba Evans Aveva ambaye alisema kuwa anaweza kujiunga na timu hiyo endapo mazungumzo yatakwenda vizuri.
Endapo Mbuyu Twitte atamwaga wino wa kuitumikia Simba itakuwa ni Mara ya pili kusaini kwenye timu hiyo.
Awali dili la Twitte lilishindikana Simba kutokana na kutokana Aden Rage aliyekuwa rais wa Simba kipindi hicho kushindwa kufata taratibu rasmi.

Comments
Post a Comment