Uncle Ngassa anukia Mbeya city


Baada ya kuzimika kwa jina lake katika ligi ya Vodacom hatimaye Mrisho Ngassa amekubali kumwaga wino kuitumikia Mbeya city.

Ngassa ambaye aliachana na Free State ya South Africa amerejea nchini na huenda akatangazwa na mbeya city muda wowote kuanzia sasa.

Msemaji wa Mbeya city Dismass Ten amesema kuwa kila kitu kipo tayari baina ya Ngasa na timu hiyo hivyo muda na saa yoyote wataweka kila kitu hadharani.

Nyota huyo wa zamani wa Yanga ataungana kwa mara nyingine na kocha Kina Phiri ambaye alikuwa naye katika timu ya Free State.

Source: Goal.com

Comments