Golikipa wa zamani wa klabu ya Simba Juma kaseja amejiunga na kwa Kagera Sugar kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kaseja ambaye alimaliza mkataba wake na Mbeya city amesajiliwa ili nguvu katika kikosi cha kocha Mecky Mexime kwenye ligi kuu ya Vodacom.
Kaseja alisaini mkataba huo ambao utamweka kwenye timu hiyo hadi ligi ya msimu huu itakapofikia tamati hapo mwakani.
Kabla ya kumalizika kwa raundi ya kwanza ya ligi kuu timu ya Kagera ilikuwa imemsimamisha golikipa wake Hussein Sharif 'casillas' ili kupisha uchunguzi kutokana na makosa ya wazi walipocheza na Yanga katika uwanja wa Kaitaba.

Comments
Post a Comment