Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa ujio wa makocha wenye heshima kama Pep Gurdiola umezidi kuongeza ushindani England.
Wenger alisema kuwa Gurdiola ni kocha mwenye jina kubwa na mwenye kuheshimika hivyo ujio umeongeza ushindani kwa kiwango kikubwa.
"Pep ni kocha mkubwa na mwenye heshima kubwa, mafanikio yake yanazidi kuifanya ligi ya England kuwa na ushindani mkubwa.
"Ni ngumu na inazidi kuwa ngumu msimu huu unatakiwa kupambana ili kufikia malengo ya ubingwa." Alisema Wenger
Ujio wa Pep Gurdiola umeamsha zaidi zaidi hisia za mashabiki ambao wameendelea kuitolea macho ligi ya England msimu huu.

Comments
Post a Comment