Klabu ya Yanga imeanza vizuri mzunguko wa pili wa ligi kuu Vodacom baada ya kuichapa JKT Ruvu bao 3-0.
Yanga chini ya kocha mpya George Lwandamina ilipata bao hizo kupitia Simon Msuva aliyefunga mara mbili huku bao lingine likiwa la kujifunga.
Yanga imesimama kileleni mwa ligi kwa pointi 36 juu ya Simba yenye pointi 35 ambayo kesho itakuwa na kibarua kizito dhidi ya Ndanda katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara.
Pia kesho kutakuwa na mchezo mkali kati ya African Lyon na Azam FC ambao utapigwa katika uwanja Uhuru.

Comments
Post a Comment