Yanga ruksa uwanja wa taifa, yasaini mkataba na serikali


Serikali imesaini mkataba na timu ya Yanga kwa ajili ya matumizi wa uwanja wa taifa pamoja na ule wa Uhuru katika mechi za kimataifa pamoja na ligi kuu ya Vodacom.

Mkataba huo umesainiwa na katibu mkuu wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdedith kwa niaba ya timu hiyo.

Mkataba huo unairuhusu Yanga kutumia viwanja kama viwanja hivyo kama viwanja vyake vya nyumbani katika mechi za ligi kuu na zile za kimataifa ikiwa ni pamoja kufanyia mazoezi.

Yanga itawajibika kulipia gharama zote endapo mashabiki wake watasababisha vurugu zitakazosababisha uharibifu wa aina yoyote kwenye viwanja hivyo.

Comments