Yanga yampotezea Chirwa, ni baada ya kumnasa mshambuliaji mwingine kutoka Zambia


Timu ya Yanga imeachana na mshambuliaji Obrey Chirwa baada ya kumsajili Winston Kalengo.

Kalengo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Zesco united anachukua nafasi ya Obrey Chirwa ambaye amepelekwa Platinums kwa Mkopo.

Yanga iliwasilisha jina la mchezaji huyo nusu saa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Winston anakuwa mchezaji wa pili wa kigeni kigeni kusajili na Yanga kwenye dirisha dogo baada ya kumsajili Justice Zulu kutoka Zambia.

Comments