Algeria yaaga michuano ya AFCON


Licha ya mshambuliaji wa Algeria Islam Sliman kutupia bao mbili lakini timu ya Algeria imeaga mashindano rasmi.

Algeria ilitoshana nguvu na Senegal baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 katika mchezo wa kufunga kundi apo Jana.

Senegal ndiye aliyeongoza kundi hilo baada ya kukusanya jumla ya pointi 7, akifuatiwa na Tunisia yenye pointi 6, Algeria pointi 2 na Zimbabwe ikiwa imevuna pointi 1.

Senegal pamoja na Tunisia zimefuzu kwenye hatua ya robo fainali.

Comments