Diego Costa aing'arisha Chelsea


Baada ya migongano ya hapa na pale hatimaye Diego Costa arejea kikosi cha kwanza na kuifungia bao timu hiyo.

Diego Costa alifunga bao la kuongoza dakika ya 45 kabla ya kuelekea mapumziko huku bao la pili likiwekwa nyavuni na Gary Cahil.

Hivi karibuni Costa alishinikiza kuwa hana furaha na timu hiyo baada ya kutishia kutimka katika ligi ya China ambayo inamwaga mpunga mzito kwa mastaa wanaocheza katika ligi za Ulaya.

Kuna kila dalili kuwa Chelsea imefikia pazuri na mchezaji huyo ambaye mshara wake utaongezwa kwa kiasi kikubwa.

Comments