Gayle awapiga chini Costa, Sanchez kwa mabao


Mshambuliaji wa Newcastle Dwight Gayle ndiye aliyefunga magoli mengi zaidi katika ligi zote za England msimu huu.

Raia huyo wa England ametupia wavuni bao 20, akiwashinda Alexis Sanchez na Diego Costa ambao wamefunga magoli 15 kila mmoja.

Gayle aliyetokea Crystal Palace na kujiunga na Newcastle msimu huu jitihada zinaiongoza timu hiyo kufanya vizuri katika ligi ya Championship na huenda 
Newcastle ikarejea tena ligi kuu.

Licha ya kuwa kipaji cha kufumania nyavu, Gayle 25 hajahusishwa kwenye kikosi cha England chini ya kocha wa sasa England Gareth Southgate.

Comments