Ivory Coast yaifata Algeria kwenye michuano ya AFCON


Mabingwa watetezi wa michuano ya AFCON Ivory Coast wamekubali kuachia ubingwa baada ya kuondoka mashindanoni hapo jana.

Ivory Coast imeondoka na pointi 2 pekee baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Morocco katika mechi ya kufunga kundi.

Wababe hao walitoshana nguvu na Togo katika mechi ya kwanza, pia Congo DRC ambayo jana imeongoza kundi baada ya kuichapa Togo bao 3-1.

Comments