Kocha wa zamani wa Barcelona na Manchester united Louis Van Gaal amekanusha taarifa zenye uvumi wa yeye kustaafu soka.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa kocha huyo alitangaza rasmi kuachana na mpango wa kuendelea kufundisha soka.
LvG 65, alisema kuwa taarifa zilizozagaa si za kweli kwa kuwa kwa sasa yupo kwenye mapumziko hadi kipindi cha majira ya joto atakapopokea ofa nyingine.
"Nipo kwenye mapumziko hadi majira ya joto na sijasema kuwa nimeachana na soka.
" Kuacha au kuendelea na soka inategemea na ofa gani nitapokea." Alisema LvG

Comments
Post a Comment