Timu ya Real Madrid imeendelea kutamba msimu huu baada ya kuichapa klabu ya Real Sociedad hapo jana kwa kipigo cha bao 3-0.
Ushindi huo unaiongoza Real Madrid kuongoza kwa pointi 4 dhidi ya mahasimu wao Barcelona kwenye msimamo wa La liga huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Barcelona ilishindwa kufurukuta mbele ya Real Betis baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 katika mchezo ambao ulipigwa mapema hapo jana.
Bao pekee zilizofungwa na Covacic, Ronaldo na Morata zimeifanya Real Madrid kuendelea kutamba kifua mbele huku wakidhihirisha huenda mahasimu wao wakasubiri sana msimu huu.

Comments
Post a Comment