Mwamuzi Mike Dean atupwa ligi daraja la kwanza


Mwamuzi maarufu katika ligi ya EPL Mike Dean hatimaye atupwa ligi daraja la kwanza na FA.

Mwamuzi huyo mwenye miaka 48 amekuwa na makosa kadhaa kwenye maamuzi yake uwanjani hivyo hali iliyopelekea kukumbana na adhabu hiyo.

Katika mechi dhidi ya West Ham na Man utd Mike Dean alimwadhibu kimakosa kwa kadi nyekundu kiungo wa West Ham Sofiane Feghouli ambaye kadi yake ilitenguliwa hapo baadae.

Pia katika mechi hiyo Mike Dean alikataa goli la wazi ambalo liliwekwa nyavuni na mshambuliaji wa Man utd Zlatan Ibrahimovic.

Desemba 16 mwaka jana Mike Dean alishindwa kumwadhibu Ross Barkley wa Everton kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu hatarishi kiungo wa Liverpool Jordan Henderson.

Mike Dean ataanza kuitumikia adhabu hiyo rasmi jumamosi ya wiki hii ambapo ataamua mechi ya kati ya Barnsley na Leeds.

Comments