MO Ibrahim hatihati kuikosa Azam leo


Timu ya Simba huenda ikashuka dimbani bila mshambuliaji Mohammed Ibrahimu dhidi ya Azam Leo.

Afya ya mchezaji huyo haijawa sawa kwa asilimia mia hivyo kuna kila dalili huenda akaikosa fainali hiyo.

Kocha msaidizi wa timu ya Simba Jackson Mayanja amesema kuwa bado wanaangalia uwezekano wa kumuhusisha nyota huyo kwenye mchezo leo.

"Bado hali ya Mohammed haijakaa sawa lakini tunategemea kuwa naye katika mechi ya leo." Alisema Mayanja

Mohammed ibrahimu amekuwa mchezaji tegemeo kwenye timu ya Simba tangu alipotua akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro

Comments