Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesema kuwa timu yao inaamini katika ubingwa na wamejipanga kushinda kila mechi iliyopo mbele yao.
Niyonzima alisema kuwa hakuna mpinzani wanaye muhofia badala yake wamejikita katika matokeo ya kupata pointi 3 katika kila mechi.
"Hiyo ndiyo nia yetu hatutaki kupoteza mechi kuanzia sasa tunahitaji kupata ubingwa kwa mara ya 3 ili tuwaoneshe kuwa sisi ni bora.
"Hatuna hofu na Simba wala Azam tunaamini katika kujituma na kupata pointi 3 muhimu katika kila mechi." Alisema Niyonzima

Comments
Post a Comment