Mshambuliaji wa Manchester city Sergio Aguero 'Kun' huenda akajiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu.
Ujio wa Gabriel Jesus katika kikosi cha Manchester city inasemekana kufungua mlango kwa Sergio Aguero ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na Real Madrid.
Licha ya kuandamwa na majeraha mara kwa mara lakini Aguero amezidi kuwa tishio anapokutana macho kwa macho na goli.
Raia huyo wa Argentina aliifungia Man city bao 2 katika ushindi wa bao 5 waliopata dhidi ya Monaco wiki iliyopita.

Comments
Post a Comment