Timu ya Arsenal na Liverpool zimetolewa kwenye nne bora ya msimamo wa ligi ya England na wachambuzi wa masuala ya soka wa kituo cha sky sports.
Katika mjadala uliofanywa na wataalamu wanne akiwemo Paul Merson, Charlie Nicholas, Phil Thompson na Matt Le Tissier wamesema kuwa Liverpool na Arsenal zinaonekana kuwa dhaifu zaidi ikilinganishwa na kiwango cha Manchester united ambayo imeanza kurudi taratibu.
Kwa upande wa Matt Le Tissier haoni nafasi ya Liverpool na Arsenal katika nne bora ya EPL msimu huu,ana amini kuwa Chelsea itakuwa bingwa, Manchester city itakamata nafasi ya pili, Tottenham namba tatu na Man utd namba 4.
Kwa upande wa Phil Thompson imekuwa tofauti kidogo, anaamini Liverpool ilipita katika upepo mbaya ambao ilikuwa ni lazima ikumbane nayo, Thompson anaamini kuwa kutokana na kiwngo cha Liverpool kilivyokuwa tishio ilikuwa ni rahisi kukamiwa. Bado ana imani kuwa Chelsea itashika usukuni wa ligi hiyo, ikifuatiwa na Man city, Tottenham na Liverpool.
Katika mjadala huo pia Charlie Nichola anaamini kuwa bado Arsenal inaweza kuwa nzuri na imara kuliko Man utd, kwa upande wake anaamini Liverpool haiwezi kuingia kwenye nne bora badala yake msimamo utakuwa kama ifuatavyo Chelsea itashikilia usukani, Man city atafuata, Tottenham pamoja na Arsenal.
Pia kwa upande wa mchambuzi wa Mwisho Paul Merson alisema kuwa haoni nafasi ya Liverpool na Arsenal kwenye msimamo wa ligi kuu kwa kuwa bado ni dhaifu ikilinganishwa na timu zingine katika sita bora. Merson anaamini kuwa Chelsea ndiye bingwa, akifuatiwa na Tottenham, Mancity pamoja Man utd.

Comments
Post a Comment