Carrick, Rooney wako fiti kuivaa fainali


Kocha wa Manchester united Jose Mourinho amethibitisha kuwa Wayne na Michael wapo fiti kucheza fainali ya kombe la EFL.

Man utd itashuka Wembley jumapili dhidi ya Southampton kutafuta mbabe atakayeondoka na taji hilo.

Mourinho alisema kuwa Wayne Rooney na Carrick wameanza wameingia mazoezini na watacheza dhidi ya Southampton.

"Rooney yuko fiti, alikosa mechi dhidi ya St Etienne kwa kuwa hakuwa tayari kwa mechi ile.
"Michael Carrick amerejea nadhani nadhani hakuna shaka juu ya afya yake." Alisema Mourinho.

Wakali hao wa Old Trafford watawakosa Henrikh Mkhitaryan na Phil Jones ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Comments