Clatternberg sasa kuachana na ligi ya England


Mwamuzi wa kimataifa wa England Mark Clatternburg ataachana na ligi ya England (PL) baada ya kupokea ofa kutoka Saudi Arabia.

Clatternberg mwenye miaka 41, amepokea ofa itakayomfanya kuwa kiongozi wa waamuzi ndani katika soka la Saudi Arabia.

Hata hivyo taarifa rasmi zimethibitisha kuwa mwamuzi huyo ataachana na England mwisho wa msimu huu.

Tayari FA imempanga mwamuzi huyo kuamua mechi ya ligi kuu kati ya West Brom na Bournemouth utakaopigwa katika dimba la Hawthorns.

Clatternberg amewahi kuchezesha mechi mbali mbali za kimataifa ikiwemo fainali ya UEFA Euro mwaka 2016 nchini Ufaransa, Kombe la dunia pamoja na fainali ya Uefa Champions league 2016/17.

Comments