Fabinho aziingiza vitani Arsenal, Man utd na Barca.


Beki anayewika katika ligi ya Ufarasa Fabinho ameziweka kwenye wakati mgumu Man utd, Arsenal na Barcelona.

Beki huyo wa Monaco yupo kwenye kiwango kizuri akiwa na uwezo mkubwa wa kupandisha mashambulizi pamoja na kufunga magoli.

Arsenal na Barcelona zinasadikika kuanza mazungumzo na raia huyo wa Brazil ambaye ameonesha wazi nia yake ya kutua Man utd.

Tangu kuondoka kwa Dani Alves Barcelona imekosa beki mzuri wa kulia, na usajili wa Fabinho (23) unaweza kuwa suluhisho kwao.

Kwa upande wa Man utd Mourinho amendelea kusaka mtu sahihi atakayeshika rasmi nafasi ya kulia ambayo nyingi inachezwa na Antonio Valencia.

Comments