Falcao ni tishio kwa Manchester city


Golikipa namba mbili wa Manchester city Willy Caballero amesema kuwa timu hiyo inatakiwa kuwa makini na Radamel Falcao katika mechi ya kesho.

Falcao 31, amerejea kwenye kiwango cha chake cha awali baada ya kuachana majeraha ya mara kwa mara yaliyokuwa yakimsibu alipokuwa na Man utd pamoja Chelsea.

Tayari nyota huyo ameshafunga mara 19 katika mechi 25 alizocheza msimu huu.

"Tunakiwa kujipanga katika mechi ya kesho, beki yetu inatakiwa kumtolea macho Falcao, ni mchambuliaji hatari kwenye timu yao." Alisema Caballero.

Comments